idan aliyasema hayo jana Ijumaa alipokuwa akihutubia Bunge, wakati akitoa mukhtasari wa hatua ambazo Uturuki tayari imechukua dhidi ya Israel au imeanza kuzitekeleza kutokana na mashambulio ya kinyama ya umwagaji damu unayoendelea kufanya utawala huo huko Ghaza, ambayo hadi sasa yamewaua shahidi zaidi ya Wapalestina 63,025.
"Tumekata kikamilifu biashara zetu na Israel, tumefunga bandari zetu kwa meli za Israel na haturuhusu meli za Uturuki kwenda kwenye bandari za Israel," ameeleza Fidan katika kikao cha dharura cha bunge kilichojadili mashambulizi ya utawala wa kizayuni dhidi ya Ghaza.
Waziri wa Mambo ya Nje wa Uturuki amebainisha kwa kusema: "Haturuhusu meli za makontena zinazobeba silaha na risasi zinazopelekwa Israel kuingia kwenye bandari zetu, na ndege kuingia kwenye anga yetu".
Wiki iliyopita, shirika la habari la Reuters liliripoti kuwa mamlaka ya bandari ya Uturuki imeanza kwa njia isiyo rasmi kuwataka mawakala wa meli kuwasilisha barua za kuthibitisha kwamba meli zao hazina uhusiano na Israel na hazibebi mizigo ya kijeshi au iliyo hatarishi inayopelekwa kwenye bandari za utawala huo ghasibu.
Kwa mujibu wa ripoti hiyo, meli zenye bendera ya Uturuki zitazuiliwa kuingia kwenye bandari za utawala wa kizayuni wa Israel.
Katika hotuba yake hiyo, Fidan aidha amesema, Israel inaifanya makusudi Ghaza iwe sehemu isiyo na watu na "kuwalazimisha watu wake waondoke."
Kadhalika amebainisha kwamba utawala huo unapinga kuibuka kwa "Syria mpya na yenye nguvu", na kuapa kuwa Ankara haitaruhusu sera hiyo kuendelea.../
Your Comment